Hizi ni kanga utakazosoma katika tovuti hii.  Soma kila kanga kabla ya kuendelea.  
Kanga za Tovuti
Akufukuzae hakwambii toka.
Amenichagua mimi uchungu wenu wa nini?
Atakalo halipati.
Furaha ya Idd shukuru Mola.
Mstahamilivu hula mbivu.
Wagombano ndio wapatano.
Usiniambie kwa mafumbo sema wazi ujibiwe.
Usife moyo.
Ungeli uliza kwanza.
Ukifurahisha wazazi utapata radhi.
Tusisahau kwetu.
Tupendane sisi kwa sisi.
Sisahau hisani japo wa zamani.
Penzi ni mauwa yapaliliwapo huchanuwa.
Nani kama mama.
Mimi na wewe hatuachani.
Lo! Hata haya huna.
Liandikwalo ndilo liwalo.
Japo mnyonge na mimi nina haki.
Dumisheni upendo, amani, utulivu na umoja.
Pokea zawadi ya Krismass na mwaka mpya.
Upendo ni tunda la roho.
Nimepewa na Mungu.
Tusidharauriane duniani tunapita.
Bahati yako ikikataa mzizi  haitafaa.
Vicheko vyenu chekeni yangu nachieni.
Usiache mbachao kwa msaala upitao.
Jiko moja haliinjiki sefulia mbili.
Hapo ni kwao.
Heri pancha ya pajero kuliko rafiki mwenye kero.